Mhe. Kikwete aipongeza Wizara kwa kukuza Sekta ya Sanaa kwa kasi, adai ina mchango mkubwa kwenye uchumi
Na John Mapepele
Rais
 Mstaafu wa Awamu ya Nne wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
 Mhe, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete ameipongeza   Wizara ya Utamaduni, 
Sanaa na Michezo  kwa  kazi kubwa inayoifanya   ambayo imesababisha kuwa
 miongoni mwa sekta zinazokuwa kwa kasi na kuchangia kwa kiasi kikubwa 
kwenye uchumi wa Taifa kwa ujumla.
Mhe.
 Kikwete ameyasema haya Usiku wa kuamkia leo Novemba 6, 2022 akiwa Mgeni
 wa rasmi kwenye uzinduzi wa albamu ya Ommy Dimpoz iitwayo Dedication 
mara baada ya kukaribishwa kutoa hotuba yake na Waziri wa Utamaduni, 
Sanaa na Michezo, Mhe. Mohamed Mchengerwa ambaye amekuwa mgeni wa 
heshima kwenye uzinduzi huo.
Amefafanua
 kuwa katika awamu hii ya Serikali inayoongozwa na Rais Samia Suluhu 
Hassan tasnina ya muziki wa kizazi kipya imekua kwa kasi na kupata 
mafanikio makubwa ukilinganisha awamu zilizopita.   
“Kila
 siku nikiangalia kwenye televisheni naona wanamuziki na wasanii wapya 
hali ambayo inaashiria kumekuwa na ukuaji wa kasi na kusababisha ajira 
kwa vijana” ameongeza Mhe. Kikwete. 
Aidha, 
amesema changamoto iliyopo kwa sasa kwenye tasnia ya muziki ni namna 
gani ya kuhakikisha wanamuziki wanapata malipo kwa kazi zinazopigwa 
kwenye vyombo vya Habari na kusisitiza Serikali kupata ufumbuzi wa 
kudumu wa suala hili ili kuwasaidia wanamuziki waweze kunufaika na jasho
 la kazi zao.
Ametoa
 wito kwa Serikali kuendelea na jitihada za kuhakikisha kuwa haki za 
wanamuziki zinalindwa kisheria ili wanamuziki waweze kufanikiwa huku 
akifafanua kuwa duniani kote   wanamuziki na wasanii wanaongoza kwa kuwa
 na vipato vikubwa.
Amempongeza 
Mtendaji Mkuu mpya wa Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) Dkt. Kedmon 
Mapana kwa kuteuliwa na Mhe. Rais kushika nafasi hiyo huku akimwelezea 
kuwa anauwezo na mchango mkubwa kwenye sekta ya Sanaa nchini na kumtaka 
 kuendelea kutoa mchango  huo kwa  faida ya  taifa la Tanzania.
Kwa
 upande wake, Waziri wa Utamaduni Sanaa na Michezo, Mhe. Mohamed 
Mchengerwa wakati akimkaribisha Rais mstaafu Kikwete ili aweze kutoa 
hotuba  yake amesema Sekta ya Sanaa  ndiyo sekta iliyoongoza  kwa  kasi 
ya ukuaji na kufafanua kuwa mwaka uliopita iliongoza  kwa kukua ambapo 
ilikuwa kwa 19% na kwamba dhamira ya Serikali  ni kutaka sekta hiyo 
kuendelea  kukua kwa kasi  ili iweze  kuchangia kwenye uchumi wa nchi  
na kutoa ajira za uhakika kwa  vijana.
Aidha
 amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu 
Hassan kwa maono yake makubwa na msukumo anaoutoa kwenye sekta hizo 
ambao umesaidia  kuleta mafaniklio makubwa   katika  kipindi kifupi cha 
utawala wake, huku pia akimpongeza  Mhe. Kikwete kwa kazi aliyoifanya ya
 kusaidia wasanii katika awamu yake. 
“Mhe. 
Rais Mstaafu nina furaha ya kueleza kuwa sekta hizi ni sekta za kuleta 
furaha  kwa wananchi na kwa kweli changamoto kwa sasa  tunayoipata  
tunaweza kusema ni suala  la kuongeza  muda wa furaha, tungependa  
kuongeza muda wa furaha  hasa kwenye majiji  hapa nchini ili wananchi 
waendelee kufurahi” ameongeza Mhe. Mchengerwa






 
 
 
Comments
Post a Comment