ZANZIBAR YANG’ARA MBIO FUPI KWENYE TAMASHA LA MICHEZO YA WANAWAKE LA TANZANITE
Na John Mapepele, Dsm Zanzibar imeibuka mbabe katika mashindano ya mbio fupi uwanja wa Benjamini Mkapa kwenye maadhimisho yanayoendelea ya Tamasha la Michezo ya Wanawake la Tanzanite leo Septemba 17, 2021ikiwa ni siku ya pili kabla ya kuzinduliwa rasmi kesho na Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan Kwa mujibu wa Mkurugenzi wa uratibu wa mbio hizo, Robert Kalyahe amesema Zanzibar imeweza kuwa bingwa kwa mbio za mita mia moja katika nafasi zote tatu ambapo amesema mshindi wa kwanza kwenye mbio hizo ni Hynes Jolini aliyetumia sekunde 11:62 akifuatiwa na Winfrida Makenji aliyetumia sekunde 11:74 na nafasi ya tatu imekwenda kwa Kazija Hassan aliyetumia sekunde12:45. Pia Kalyahe amesema katika mbio za mita mia mbili nafasi zote tatu zimenyakuliwa na washindi kutoka Zanzibar ambapo amesema Emma Hossea amenyakua nafasi ya kwanza kwa kutumia sekunde 24:82 na nafasi ya pili imechukuliwa na Nasra Abdallah aliyetumia sekunde 25:55 wakati nafasi ya tatu imekwenda kwa Neema Ally a...

Comments
Post a Comment