Mhe. Mchengerwa- Tanzania na Real Madrid wajadili ushirikiano katika michezo.
Na John Mapepele
Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Mohamed Mchengerwa amefanya majadiliano ya awali na uongozi wa juu wa Klabu ya Real Madrid ya Hispania kuhusu kufanya ushirikiano katika kukuza vipaji vya Soka baina ya Klabu hiyo na Tanzania.
Mazungumzo hayo yamefanyika leo Oktoba 10, 2022 kwa njia ya mtandao ambapo wamejadili kufanya uwekezaji mkubwa kwenye kuibua vipaji vya wachezaji wachanga na kuwakuza kuanzia kwenye akademi za michezo.
Mhe. Mchengerwa amesema Klabu hiyo imekubali kushirikiana na Tanzania kuendeleza vipaji vya vijana ili kuwapata wachezaji bora wa kimataifa kwa manufaa ya pande zote mbili.
Mbali na kufanya uwekezaji mkubwa katika kuibua vipaji, pia imejadiliwa kushirikiana katika kutumia michezo kutangaza utalii wa Tanzania kwa kutumia mitandao mbalimbali ya Klabu hiyo kongwe duniani.
Mhe. Mchengerwa amesema Tanzania ina fursa kubwa ya kutumia michezo kuitangaza nchi kimataifa na kuinua uchumi wake

Comments
Post a Comment