RAIS SAMIA AWAPA SALAMU TEMBO WARRIORS, MHE. MCHENGERWA ATOA AHADI NONO WAKISHINDA

 

Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Mohamed Mchengerwa amesema Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan anaipongeza  Timu ya Taifa ya Tembo Warriors kwa kufuzu kombe la Dunia kwa watu wenye ulemavu linalotarajiwa kufunguliwa Septemba 30, 2022 na kuitaka kutanguliza uzalendo na kujituma ili warudi na Kombe nyumbani.

Akizungumza kwa njia ya simu kupitia kwa Katibu Mkuu Dkt. Hassan Abbasi Waziri Mchengerwa amesema Serikali ya Tanzania ipo pamoja na wao katika kila hatua na ndio maana Rais ameridhia viongozi wa Wizara kuambatana nao katika fainali hizo.

“Rais na Serikali yenu ipo pamoja na nyinyi, nendeni mkalipiganie Taifa, onesheni uzalendo na kuhakikisha mnarudi na Kimbe nchini na hiyo itakuwa ni zawadi kwake Mhe. Rais na Tanzania kwa ujumla”’ amefafanua Mhe. Mchengerwa.

Aidha ameahidi zawadi nono kwa timu hiyo ikiwemo shilingi milioni 40 endapo watafuzu robo fainali, shilingi milioni 80 wakifuzu kucheza nusu fainali na shilingi milioni 100 wakifanikiwa kufuzu fainali za michuano hiyo.

Ameongeza kuwa akiwa nchini Uturuki anatarajia kufanya mazungumzo na Waziri wa Michezo na kusaini mkataba wa mashirikiano baina ya Tanzania na Uturuki katika sekta za michezo ili kusaidia kukuza sekta hiyo nchini Tanzania.

Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Dkt. Hassan Abbasi amewaasa wachezaji kuzingatia nidhamu, umoja na kumtanguliza Mungu na kusema kuwa Serikali ipo kuhakikisha kila kitu kinakwenda vizuri.

Kwa upande wake Nahodha wa  timu hiyo Steven Manumbu ameahidi ushindi kwa Mhe. Waziri na kusema kuwa timu ipo tayari kwa ajili ya kuipambania nchi yao.

Naye kocha wa timu hiyo Salvatory Edward amesema morali ya wachezaji hao ipo juu  pia wanatambua nini wanatakiwa kufanya



Comments

Popular posts from this blog

ZANZIBAR YANG’ARA MBIO FUPI KWENYE TAMASHA LA MICHEZO YA WANAWAKE LA TANZANITE

Mhe. Mchengerwa- Serikali kuwashirikisha wadau kwenye mnyororo wa thamani wa utalii