Posts

Showing posts from February, 2023

Mhe. Mchengerwa- Serikali kuwashirikisha wadau kwenye mnyororo wa thamani wa utalii

Image
  Na John Mapepele Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Mohamed Mchengerwa amesema Serikali imedhamiria kufanya kazi kwa pamoja na wadau mbalimbali wa utalii nchini kwa ajili ya kuimarisha mahusiano ya serikali na wadau (Public Private Partnership) ili kufikia kwa haraka   lengo la  kuwapata  watalii  milioni tano hatimaye  kuchangia  kwenye uchumi wa nchi. Akizungumza kwenye Tamasha la Kwanza la Biashara la Wadau wa Utalii leo, Februari 23, 2023 lililopewa  jina la “The Z sumit” ambapo Rais wa Zanzibar, Mhe. Hussein Mwinyi amekuwa Mgeni Rasmi, Mhe. Mchengerwa amesisitiza kuwa  dhamira ya serikali kwa sasa ni kuwashirikisha wadau  wote  kwenye mnyororo wa thamani wa utalii ili kutoa huduma  ya kiwango cha kimataifa kitakachowavutia watalii kuja kujionea vivutio mbalimbali vya utalii hapa nchini. Aidha, amemhakikishia Mhe. Rais Mwinyi kufanya kazi kwa karibu na Waziri anayesimamia sekta ya Utalii kwa upande wa Zanzibar katik...

Serikali yawazawadia Watanzania Sports Arena siku ya valentine.

Image
Na John Mapepele Leo ikiwa ni siku ya wapendanao duniani (valentine) Wizara ya Utamaduni Sanaa na Michezo  imepokea kutoka Shirika la Nyumba ( NHC) eneo la ekari 12  Kawe Jijini Dar es salaam litakalojengwa Ukumbi wa Kimataifa wa kisasa wa Michezo (Sports Arena). Akizungumza na Wanahabari  mara baada ya kukabidhiwa, Waziri wa utamaduni sanaa na Michezo, Mhe. Mohamed Mchengerwa aliyeambatana na Katibu Mkuu Dkt. Hassan Abbasi amesema, Wizara inakwenda kulikabidhi eneo hilo mwezi Machi kwa Mkandarasi na ujenzi utachukua muda wa miezi 08 hadi 10  umekamilika. Aidha, Mhe. Mchengerwa ameeleza kuwa dhamira ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,  Dkt.Samia Suluhu Hassan ni kuhakikisha sekta ya burudani na michezo zinakuwa  Sekta zinazochangia kwa kiasi kikubwa kwenye pato la Taifa na wananchi wananufaika nazo Amesisitiza kuwa watanzania wana kiu ya kuona Ukumbi wa Kimataifa wa michezo kama zilivyo nchi zingine unajengwa nchini Tanzania. Amefafanua kuwa Kujengw...

TAARIFA YA UFAFANUZI KUTOKA WIZARA YA UTAMADUNI,SANAA NA MICHEZO

Image
 

WAZIRI MCHENGERWA KUPOKEA TATU KUBWA YA KIHISTORIA FEBRUARI 3,2023

Image
  ************************* WAZIRI wa Utamaduni Sanaa na Michezo Mohamed Mchengerwa anatarajiwa kupokea Mageuzi matatu ya kihistoria katika wizara hiyo siku kesho Februari 03,2023 katika ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano Mwalimu Nyerere (JNICC) Jijini Dar es salaam. Akizungumza na Wanahabari Leo Februari 02,2023 Ofisi za Baraza la Sanaa Taifa (BASATA) Katibu Mkuu wa Wizara ya Sanaa na Utamaduni Dkt.Hassan Abbas amesema Wizara hiyo siku ya kesho inaenda kuandika historia kubwa 3 zenye mchango mkubwa kwa taifa la Tanzania. "Ni lazima nchi ya Tanzania tuwe na Muziki ambao unalimtambulisha taifa hivyo tuliteua kamati ambayo iliongozwa na watu wabobezi katika kuhakikisha mdundo unapatikana kwa kuzingatia mdundo huo haupotezi vionjo vya kitamaduni ya kitanzania." Hata Katibu mkuu ameeleza kuwa Kamati hiyo ilisheheni watayarishaji mbalimbali na wadau wakubwa wa Kimuziki. "Kamati hii iliongozwa na Mwenyekiti Dkt.Kedmon Mapana nafikiri umahiri wake unafahamika ,Masoud Masoud manji ...