Posts

Showing posts from October, 2022

Waziri Mchengerwa atoa siku 30 kwa BMT kutengeneza mifumo ya kusajili ya kielektoniki

Image
  Na John Mapepele  Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Mohamed Mchengerwa amelielekeza Baraza la Michezo la Taifa (BMT) kuhakiksha ndani ya mwezi mmoja linatengeneza mfumo wa kieletroniki wa kusajili vyama vya michezo ili kuondoa usumbufu kwa wadau unaojitokeza. Mhe. Mchengerwa ameyasema  haya  leo Oktoba 27, 2022 wakati akizindua program ya “Mpira Fursa” inayoratibiwa na Taasisi ya Karibu Tanzania (KTO) na kugawa  vifaa vya michezo kwa  Vyuo vya Wananchi vya  Maendeleo 54 kote nchini na shule za msingi 86.   Ameutaka uongozo wa shule ambazo zitabahatika kupata vifaa vya soka, kuwaruhusu wasichana kucheza soka na kuvitumia vifaa hivyo kwa uangalifu na kwa madhumuni yaliyokusudiwa.   Ameipongeza KTO kwa kuanzisha program hiyo ya kupeleka  michezo  katika vyuo vya  wananchi  vya maendeleo na shule za msingi huku akifafanua kuwa  huo ni utekelezaji wa  maono ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanza...

Waziri Mchengerwa azindua zoezi la kitaifa la kusaka na kuibua vipaji "mtaa Kwa mtaa."

Image
Na John Mapepele Waziri wa Utamaduni,  Sanaa na Michezo, Mhe. Mohamed Mchengerwa leo Oktoba 16, 2022 amezindua  zoezi la  kitaifa la  kuibua na kusaka vipaji  vya Sanaa la "Mtaa kwa Mtaa" eneo la  Ikwiriri wilayani Rufiji, zoezi ambalo litafanyika nchi nzima. Akizindua zoezi hilo katika eneo la Ikwiriri, Mhe. Mchengerwa amesema eneo linalofuata baada ya uzinduzi wa leo ni Mkoa wa Arusha ambapo litafanyika kila mtaa ili kuibua vipaji kwenye sanaa. Amewataka watanzania  wenye vipaji vya Sanaa kujitokeza wakati wa zoezi hilo likiendelea  ili waweze kuendelezwa baada ya kuibuliwa, huku akisisitiza  kauli ya Kipaji chako ndiyo mtaji wako. "Ndugu zangu hii ni ndoto ya Mheshimiwa Rais wetu, Rais anatamani kuona misingi iliyowekwa na Baba wa Taifa, Mwalimu Nyerere ya kuthamini na kuendeleza Sanaa inaendelezwa ili kuwanufaisha vijana" amesisitiza,  Mhe. Mchengerwa   Amezitaka mamlaka za wilaya na mikoa kote nchini kusaidia  kuibua ...

Mhe. Mchengerwa- Tanzania na Real Madrid wajadili ushirikiano katika michezo.

Image
  Na John Mapepele Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Mohamed Mchengerwa amefanya majadiliano ya awali na uongozi wa juu wa Klabu ya Real Madrid ya Hispania kuhusu kufanya ushirikiano katika kukuza vipaji vya Soka baina ya Klabu hiyo na  Tanzania. Mazungumzo hayo  yamefanyika leo Oktoba 10, 2022 kwa njia ya mtandao ambapo wamejadili  kufanya uwekezaji mkubwa kwenye kuibua vipaji vya wachezaji wachanga na kuwakuza kuanzia kwenye akademi za michezo. Mhe. Mchengerwa amesema Klabu hiyo imekubali  kushirikiana na  Tanzania  kuendeleza vipaji vya vijana ili kuwapata wachezaji bora wa kimataifa  kwa manufaa ya pande zote mbili.  Mbali na kufanya uwekezaji mkubwa katika kuibua vipaji, pia imejadiliwa kushirikiana katika  kutumia michezo kutangaza utalii  wa Tanzania kwa kutumia mitandao mbalimbali ya Klabu hiyo kongwe duniani. Mhe. Mchengerwa amesema Tanzania ina fursa  kubwa  ya kutumia michezo kuitangaza nchi kimataifa ...