Posts

Showing posts from May, 2023

USHIRIKI WA BRELA KATIKA MAADHIMISHO YA SIKU YA WAFANYAKAZI DUNIANI

Image
  Maafisa wa Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA), wakiwa  katika maadhimisho ya siku ya Wafanyakazi Duniani (Mei Mosi) mkoani Morogoro na jijini Dar es Salaam ambapo kitaifa yamefanyika katika uwanja wa Jamhuri mkoani Morogoro.  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ndiye aliyekuwa mgeni rasmi katika maadhimisho ya kitaifa. Jijini Dar es salaam maadhimisho yamefanyika kimkoa katika Uwanja wa  Uhuru uliopo Wilaya ya Temeke.  Kauli mbiu kwa mwaka huu ni  “Mishahara Bora na Ajira za Staha ni nguzo kwa maendeleo ya Wafanyakazi" Wakati ni Sasa!    Mkuu wa Wilaya ya Temeke Mhe. Mwanahamisi Munkunda, ndiye aliyekuwa Mgeni Rasmi akimwakilisha  Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam.

Royal Tour imeleta mazao lukuki ya utalii- DK Abbasi

Image
   Na John Mapepele Katibu Mkuu wa Maliasili na Utalii na Mwenyekiti wa Kamati ya Kuitaingaza Tanzania ya Royal Tour, Dkt. Hassan Abbasi amesema wakati Tanzania imetimiza mwaka mmoja toka Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan atoke ofisini na kucheza filamu ya Royal Tour, kumezaliwa mazao mbalimbali ya utalii hapa nchini. Dkt. Abbasi ametoa kauli hiyo leo Mei 1, 2023 wakati akihitimisha mjadala wa kitaifa kwenye mtandao (Zoom Meeting) uliojumuisha wadau mbalimbali wa utalii  duniani na  kurushwa mubashara  ya  mitandao na vyombo  mbalimbali vya habari ulioangazia mafanikio  yaliyopatikana  katika kipindi cha mwaka mmoja wa Royal Tour. Amesema kutokana shuhuda nyingi zilizotolewa na wadau kuwa  kumekuwa na mafanikio makubwa katika kipindi kifupi tangu Roal Tour ilipozinduliwa  inapaswa  kila mtanzania kuwa balozi wa  kuitangaza Tanzania ikiwa ni mkakati wa kuunga mkono juhudi za Serikali ya awamu...