Posts

Showing posts from July, 2022

Mhe. Mchengerwa atembelea miundombinu ya Michezo Uingereza

Image
  Na John Mapepele, Leicester Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo. Mhe, Mohamed Omary Mchengerwa ametembelea miundombinu ya michezo nchini Uingereza na kufanya mazungumzo na wamiliki wake lengo likiwa ni kuboresha miundombinu    ya michezo nchini. Katika ziara hiyo aliyoifanya Julai 30, 2022, Mhe. Mchengerwa ametembelea kiwanja cha   King Power na St Mary’s kinachomilikiwa na klabu ya Southampton na kujionea miundombinu   mbalimbali ya michezo na kujifunza namna  bora ya kuiendeleza na usimamizi wa miundombinu hiyo.  “Tumejifunza mambo  mambo mengi makubwa ambayo sisi pia tunaweza kuyaiga na kuyaboresha  kutoka kwa wenzetu hawa ambao wamepiga hatua kubwa kwenye anga ya michezo na sisi tukapiga hatua  ya haraka” amefafanua Mhe. Mchengerwa  Akiwa kwenye ziara hiyo Mhe. Mchengerwa alipata  fursa  ya kushuhudia   fainali za kombe la ngao ya jamii  mchezo uliochezwa  kwenye  uwanja wa  ...

Dkt.Migiro, amshukuru Rais, aipongeza Wizara kwenye michezo

Image
  Na John Mapepele, London Balozi wa Tanzania, nchini Uingereza. Dkt, Asha Rose Migiro amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,  Mhe. Samia Suluhu Hassan kwa kutoa jicho la pekee kwenye sekta ya  michezo. Mhe Balozi Migiro ametoa kauli hiyo leo Julai 29, 2022  nchini Uingereza kwenye mashindano ya Michezo ya  Jumuiya ya Madola ambapo Tanzania inashiriki. "Hapa napenda kusema  kwa dhati kama Balozi mwanamke wa Tanzania hapa Uingereza kuwa  namshukuru Mhe. Rais kwa kutoa kipaombele kwenye michezo na sasa tunaona mafanikio makubwa kwenye michezo ya wanawake' ameongeza Mhe. Migiro Hadi sasa tayari timu ya taifa ya soka ya wanawake  chini ya umri wa miaka 17 ( Serengeti Girls) na timu ya taifa ya wanawake ya  Kabbadi zimefuzu kuingia kwenye  mashindano ya dunia ya michezo  hiyo. Aidha, amempongeza wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo kwa kazi nzuri inayofanya ya kuitangaza  Tanzania duniani kupitia michezo. Akizungumzia...

Tutaishangaza dunia- Timu ya Jumuiya ya Madola

Image
  Na John Mapepele, Birmingham - Uingereza Kocha Mkuu Timothy Kingu wa kikosi cha ndondi kinachoiwakilisha Tanzania kwenye mashindano ya Jumuiya ya Madola ambayo yanaanza rasmi leo Julai 28,2022 amemhakikishia Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan na watanzania wote kurejea na medali za ushindi kwenye mchezo huo kwa kuwa wamepata maandalizi ya kutosha. Akizungumza katika kambi ya wachezaji hao jijini Birmingham, Uingereza amesema wachezaji wake wamepikwa vizuri na watapata hamasa ya kutosha tayari kwa ajili ya pambano lililopo mbele yao. Aidha, amesema hamasa kubwa inayotolewa na Rais Samia Suluhu Hassan na Waziri anayesimamia Michezo nchini, Mhe Mohamed Mchengerwa na wadau mbalimbali kwa sasa zinawafanya wawe na ali na nguvu zaidi ya kushindana kufa na kupona kwenye mashindano haya. Hadi sasa, tayari Mabondia wawili wa Tanzania Yusuf Changarawe na Kassim Mbundwike wameingia robo fainali za mchezo ya Jumuiya ya Madola inayoanza rasmi leo jijini Birmingham, Uingereza Bondia wa tatu wa Tanza...

Waziri Mchengerwa aitembelea timu ya Jumuiya ya madola, aifunda

Image
  Na John Mapepele, Birmingham Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo. Mhe Mohamed Mchengerwa ameitembelea timu ya wachezaji wa Tanzania inayoshiriki mashindano ya Jumuiya ya Madola   Birmingham nchini Uingereza na kuitaka kupambana kufa na kupona ili kurejea na medali. Mhe. Mchengerwa ameyasema haya leo Julai 27, 2022 kwenye kambi ya timu hiyo huku akisisitiza kuwa watanzania wakiongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Mhe Samia Suluhu Hassan wana matumaini makubwa na timu hiyo hivyo hawana budi kulinda heshima kubwa waliyopewa na taifa kwa ujumla. "Nawaomba tangulizeni uzalendo ili tuweze kushinda, hii ni vita  tunahitaji kupambana bila kujali idadi yetu wala kitu chochote. Tutashinda." Amesisitiza Mhe. Mchengerwa Aidha,  amesema dhamira ya Serikali kwa sasa ni kuinua  na kuendeleza michezo kwa kuwa michezo ni chanzo. Ha ajira na uchumi kwa taifa. " kwa kutambua hilo ndiyo maana kwa mara ya kwanza Serikali  imeamua kutoa fedha nyingi kwa w...

TAARIFA YA PONGEZI KUTOKA WIZARA YA UTAMADUNI SANAA NA MICHEZO

Image

Mhe. Mchengerwa Aeleza Umuhimu wa Kuwekeza katika Michezo

Image
  Na Mwandishi wetu, Birmingham Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Mohamed Mchengerwa ameeleza kuwa, uwekezaji  katika michezo ni muhimu kwa kuwa unasaidia kutoa ajira na kukuza uchumi wa nchi. Mhe. Mchengerwa ameeleza hayo leo Julai 27, 2022 katika Mkutano wa Mawaziri wa Michezo wa Nchi za Jumuiya ya Madola unaofanyika Birmingham Uingereza, ambapo amesema ni wakati sasa kwa nchi zinazoendelea kutoa kipaumbele katika michezo kama zinazofanya katika Sekta zingine. "Ni wakati sasa wa kuipa Sekta ya michezo kipaumbele, tuondoe dhana ya kuchagua ikiwa tunataka kujenga miundombinu ya michezo na afya tunachagua afya, bali michezo pia tuipe kipaumbele kwakua katika Dunia ya leo,   michezo ni Sekta ambayo inatoa ajira na kukuza pato la nchi" alisema Mhe.Mchengerwa. Ameongeza kuwa, ushirikiano kati ya Serikali na Sekta binafsi utasaidia Sekta hiyo kukua zaidi, huku akiwakaribisha wanachama wa Jumuiya hiyo kuwekeza katika michezo nchini Tanzania. Mhe. Mchengerwa ametum...

Waziri Mchengerwa aongoza kikao cha ujumbe wa Tanzania, Birmingham Uingereza

Image
  Na John Mapepele Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo. Mhe,  Mohammed Mchengerwa  ameongoza kikao cha maandalizi ya ujumbe wa Tanzania katika kikao cha Mawaziri wa Michezo wa Jumuiya ya Madola kitakachoanza leo Julai 26 mjini Birmingham, Uingereza.  Kikao hicho ni maandakizi mahususi kabla ya uzinduzi rasmi wa mashindano ya michezo ya Jumuiya ya Madola ya mwaka huu yanayofanyika nchini Uingereza huku Tanzania ikiwa imeshiriki katika michezo hiyo. Katika mashindano hayo kwa mara ya kwanza Serikali imetoa  motisha kubwa kwa wachezaji watakaofanya vizuri na kurejea na tuzo nchini. Mhe. Mchengerwa amesema dhamira ya Serikali ni kuhakikisha   michezo inatumika kikakamilifu kuitangaza Tanzania kimataifa. Aidha, amesema michezo ni ajira na uchumi mkubwa ambapo amesisitiza wachezaji wote kuwa wazalendo kujituma kufa na kupona kwa ajili ya taifa la Tanzania. Amepongeza jitihada kubwa zinazofanywa na Serikali chini ya Rais Samia Suluhu Hassan za kuleta mapind...

Rais Samia awamwagia madola wachezaji Jumuiya ya Madola- Mhe Mchengerwa

Image
  Na John Mapepele Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo. Mhe, Mohamed Mchengerwa  amesema  Serikali inakwenda kutoa zawadi kwa wachezaji wote watakaoleta medali za mashindano ya madola yanayoanza nchini Uingereza hivi karibuni kama hamasa maalum kwa wachezaji. Amesema kwa mara ya kwanza  kabisa Serikali imeandaa zawadi dola  10000 kwa mshindi atakayerejea na medali ya dhahabu na  dola 7000 kwa mshindi wa medali ya fedha  na mshindi atakayeshinda  medali ya shaba atapata dola za kimarekani 5000. Mhe, Mchengerwa ameyasema hayo leo Julai 20, 2022 kwenye hafla ya  kuwaaga wachezaji wa Tanzania wanaokwenda kushiriki mashindano ya Jumuiya ya Madola nchini Uingereza. Katika hafla hiyo iliyofanyika Ukumbi wa Uwanja wa Mkapa jijini Dar es Salaam amewataka wachezaji kuweka uzalendo mbele na kuwataka kurudi na medali. Amefafanua kuwa watambue kwamba dhamira ya Serikali kwa sasa ni kufanya mapinduzi makubwa ambapo amesisitiza kuwa watanzania wamechoka w...

Mhe. Mchengerwa amwaga vifaa vya michezo shule zote wilaya ya Rufiji, aanzisha ligi ya Sensa

Image
  Na John Mapepele Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo na Mbunge wa Jimbo la Rufiji.  Mhe, Mohamed Omary Mchengerwa ametoa vifaa vya michezo kwa shule zote za msingi na Sekondari na wanafunzi wanamichezo wote  wanaoshiriki kwenye mashindano ya michezo kwa shule za Msingi (UMITASHUMTA) na Mashindano  ya Shule za Sekondari (UMISSETA) kwa mwaka 2022 Wilaya ya Rufiji. Mhe. Mchengerwa amekabidhi  vifaa hivyo kwa Mkuu wa Wilaya ya Rufiji Julai 17, 2022 kwenye  shule ya Sekondari ya Ikwiriri   Wilaya ya Rufiji ambapo amesema ameamua  kufadhili vifaa hivyo katika Wilaya ya Rufiji ili kuiendeleza michezo kwa kuwa michezo ni biashara  na ajira kubwa  kwa vijana. “Nimeamua kusaidia vifaa hivi kwakuwa natambua  kwa sasa michezo ni miongoni mwa chanzo cha ajira na biashara kubwa duniani hivyo ni vema kufanya michezo kwa umakini mkubwa ili kujipatia ajira” amefafanua Amewataka wachezaji hao kuwa na nidhamu na kujituma kwa kufanya mazoezi i...

Mhe. Mchengerwa kuunda Kamati Maalum ya kuandaa mdundo wa kitanzania

Image
  Na John Mapepele Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo. Mhe, Mohamed Mchengerwa amesema anakwenda kuunda kamati maalum kwa ajili ya kuratibu uzalishaji mdundo  wa muziki wa  kitanzania ambao utaitangaza  Tanzania Duniani.   Mhe. Mchengerwa ameyasema hayo leo Julai 13, 2022 alipotembelea studio ya kuzalisha kazi za sanaa ya Wanene na kufanya majadiliano na wafanyakazi wa studio hiyo iliyopo jijini Dar es Salaam. “Dhamira ya Serikali kwa sasa ni kuwa na mdundo utakaoitambulisha nchi yetu kimataifa ili kuuza utamaduni wa nchi yetu kwenye mataifa mbalimbali duniani” amesisitiza Mhe. Mchengerwa. Amesema Kamati hiyo maalum itaundwa na walimu wabobezi   kutoka vyuo vikuu, wazalishaji wa Muziki, wanamuziki pamoja na viongozi wa kimila(machifu). Amesema Tanzania imebahatika kuwa na utajiri wa utamaduni ambao kama utatumika vizuri kutengeneza midundo  ya miziki kama ilivyo kwa nchi mbalimbali duniani utasaidia  kuitangaza  Tanzania na ...

Mhe.Mchengerwa afanya ziara BASATA, ampa maelekezo mahususi, Dkt. Mapana

Image
  Na John Mapepele Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo. Mhe, Mohamed Mchengerwa amemtaka Katibu Mtendaji wa Baraza la Sanaa *(BASATA)* nchini  Dkt. Mapana kurudisha hadhi ya sekta ya Sanaa nchini kwa kuweka mikakati itakayosaidia kukuza sekta na kuchangia mapato ya wasanii na uchumi wa taifa kwa ujumla. Mhe. Mchengerwa ameyasema haya leo Julai 12, 2022 alipotembelea Ofisi ya BASATA  na kutoa maelekezo kwa Mtendaji Mkuu huyo wa BASATA aliyeteuliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Mhe, Samia Suluhu Hassan. Baadhi ya maelekezo ambayo ametaka yafanyiwe kazi mara moja ni pamoja na kuziba mianya yote ya rushwa na upotevu wa mapato ambapo amesisitiza kuwa endapo utadhitiwa utasaidia kuongeza fedha nyingi Serikalini. Pia amemtaka kuwa mbunifu wa mambo katika kuongoza taasisi hiyo ili kuja na mapinduzi chanya katika sekta hiyo. "Katika wakati wa sasa ni muhimu kuipanga taasisi yako na kuwa na wataalam bobezi kwenye kila eneo kama wachumi, wataalam wa masoko, sheria na...

Mhe. Mchengerwa awatakia watanzania Idd njema

Image
  Na John Mapepele Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo. Mhe, Mohamed Mchengerwa amewatakia heri ya sikukuu ya Idd waislam na watanzania wote. Salam hizo amezitoa leo Julai 10, 2022 wakati wa swala na baraza la Eid El - Adh'haa kitaifa  lililofanyika jijini Dar es Salaam  kwenye Msikiti wa Mfalme wa Morocco Muhammad VI Bakwata  Makao Makuu. Mhe. Mchengerwa amewata watanzania kusherehekea kwa amani na utulivu huku wakimtanguliza Mwenyezi Mungu.  Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Mhe Kassim Majaliwa. Majaliwa  ndiye mgeni rasmi. Amesema  siku hii ni ya upendo kwa watu wote na ambapo inatakiwa kusherehekewa kwa upendo, amani na mshikamano. Amewapongeza  viongozi wa dini na vyombo vya habari kulielezea zoezi la sensa ya watu na makazi na kuwataka wananchi wote kushiriki. Aidha, amepongeza taasisi za dini kuendelea kutoa huduma mbalimbali za afya na maji. Pia Mhe. Waziri Mkuu ametumia fursa hiyo kutoa ufafanuzi wa suala la uhamaji wa hia...